Google Gemini kwenye Wear OS - Kiratibu chako muhimu kinachotumia AI mkononi mwako
Gemini kwenye Wear OS ni kiratibu chetu muhimu kinachotumia AI kilicho kwenye saa yako. Zungumza tu kama kawaida ili ufanye mengi popote ulipo. Gemini inaweza kutekeleza majukumu kwenye programu mbalimbali, kujibu maswali na kukumbuka mambo muhimu kwa niaba yako.
Jaribu kuiuliza Gemini ili:
Uendelee kuwasiliana: “Tuma ujumbe kwa Nadia umwambie samahani nitachelewa”
Upate maelezo: “Mgahawa ambao Emily aliutaja katika barua pepe kuwa tutakuwa na chajio leo uko wapi?”
Idhibiti muziki: “Nitayarishie orodha ya kusikiliza ninapokimbia maili moja ndani ya dakika 10”
Ikumbuke maelezo: “Kumbuka nimeegesha gari ghorofa ya 2, nafasi ya 403”
Programu ya Gemini inapatikana kwenye vifaa, lugha na nchi mahususi. Inahitaji saa oanifu ya Wear OS iunganishwe na kifaa oanifu. Kagua usahihi wa majibu. Inaweza kuhitaji muunganisho wa intaneti na kuweka mipangilio. Matokeo ni kwa madhumuni ya mifano na yanaweza kutofautiana.
Buni kwa kuwajibika:
https://policies.google.com/terms/generative-ai/use-policy
Angalia orodha kamili ya lugha zinazotumika na nchi inakopatikana hapa:
https://support.google.com/?p=gemini_app_requirements_android
Ukichagua kutumia programu ya Gemini, itachukua nafasi ya programu ya Kiratibu cha Google kama kiratibu cha msingi katika saa yako. Baadhi ya vipengele vinavyotumia sauti vya programu ya Kiratibu cha Google bado havipatikani kupitia programu ya Gemini. Unaweza kubadilisha ili utumie programu ya Kiratibu cha Google kwenye mipangilio.
Ilisasishwa tarehe
31 Jul 2025